Viongozi wa kauti ya
Nakuru wamekaribisha hatua ya baraza la mawaziri ya kutenga shulingi bilioni
sita nukta tano za kuendeleza mradi wa eneo lililotengewa ujenzi wa viwanda
mjini Naivasha.
Wakiongozwa na gavana
Lee Kinyanjui, viongozi hao wamesema hatua hiyo itapelekea vijana wengi kupata
nafasi za kazi na kusema kwa sasa mradi wa reli ya kisasa ya SGR inakaribia
kukamilika tukio ambalo litabadilisha maisha ya wengi.
Kinyanjui amesema kwa
sasa serikali yake ilikuwa ikifanya mazungumzo na wawekezaji wa humu nchini na
wale wa nchi za nje kwa madhumuni ya kuanzisha viwanda eneo hilo.
Naye mwakilishi wa wadi
ya lake View mjini humo Karanja Mburu amesema wengi watanufaika na miradi hiyo
eneo la Mai mahiu na kuongeza kuwa wakazi walikuwa wakiunga mkono miradi ya
serikali kuu eneo hilo.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.