Kinachowatofautisha
matajiri na masikini kwenye fedha siyo kipato wanachoingiza, bali ni
mtazamo walionao kwenye kipato wanachoingiza.
Masikini
wana mtazamo wa kufanyia kazi fedha, na ndiyo maana wanachofikiria wao
ni kuajiriwa na kufanya kazi muda wao wote na kulipwa kulingana na kazi
waliyofanya. Mtazamo huu unawaingizia kipato kizuri, lakini kinakuwa na
ukomo. Kwa sababu una masaa 24 tu kwenye siku yako na una miaka michache
ya kuweza kufanya kazi kwa juhudi, mwili unachoka na huwezi kujituma
tena.
Matajiri
wana mtazamo wa kuifanya fedha iwafanyie wao kazi, ndiyo maana wao
hufikiria biashara na uwekezaji zaidi. Wanatengeneza mfumo ambao unaweza
kuzalisha fedha bila ya wao kuwepo moja kwa moja. Mwanzoni mambo huwa
ni magumu kwao, kwa sababu kipato kinakuwa siyo cha uhakika kama kwa
wale walioajiriwa, lakini mfumo wanaoujenga unapokamilika, wananufaika
sasa.
Ukichukua
watu wawili, ambao wana umri sawa, mmoja kaanzisha biashara na kuijenga
vizuri na mwingine kaajiriwa, wote wakajituma kwa miaka 20, ukija
kuwaangalia, wa biashara atakuwa anazidi kukuza kipato chake huku wa
ajira atakuwa anazidi kuzama kwenye madeni.
Huo ndiyo uhalisia, japo umekuwa hauoneshwi wazi, kwa sababu watu hawataki ujue ukweli, ili waendelee kukutumia ipaswavyo.
Sasa
mimi rafiki yako, nimejipa wajibu wa kuhakikisha wewe unapata maarifa
sahihi ili uweze kufanya maamuzi sahihi ya maisha yako. Na moja ya
maarifa ambayo wewe unayahitaji sana ni upande wa FEDHA.
Watu
wengi hawana maarifa sahihi ya kifedha, wengi wanaishi kifedha kwa
mazoea, kama ambavyo wazazi wao walikuwa wanaishi, na ndiyo maana
utakuta waliotokea kwenye umasikini wanaendelea kubaki kwenye umasikini.
Kukusaidia wewe uondoke kwenye mtego huo, Nimeandika kitabu kizuri sana kwako, kinaitwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
Kitabu
hiki kina maarifa yote ya kifedha, kuanzia kuongeza kipato, kudhibiti
matumizi, kuweka akiba, kuwekeza, kuondoka kwenye madeni, kuwa na
biashara, kulinda utajiri wako, kuwafundisha watoto elimu ya kifedha,
kuandaa wosia na kutoa kwa wenye uhitaji.
Ni
kitabu ambacho kitakupa msingi wa kufanya maamuzi sahihi kifedha,
ambayo yatakusaidia sana kuweza kupiga hatua kwenye maisha yako.
Kama
bado hujasoma kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, hebu chukua
hatua leo rafiki yangu. Kitabu kinapatikana kwa nakala ngumu (HARD COPY)
na utaweza kuletewa au kutumiwa popote pale ulipo nchini Tanzania.
Kupata kitabu, piga simu 0678 977 007 leo hii na upate kitabu na utakuwa umepiga hatua ya kwanza kuondoka kwenye umasikini.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Kocha Dr. Makirita Amani,
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.