Rafiki yangu mpendwa,
Zipo
siri nyingi sana za mafanikio, na japo zinaitwa siri, huwa ni vitu vya
wazi, kabisa. Ila kwa kuwa wengi hawapo tayari kuchukua hatua
wanazopaswa kuchukua ili kufanikiwa basi hatua hizo zinaonekana ni siri.
Siri
za mafanikio zilizozoeleka ni kufanya kazi kwa juhudi, kuwa mbunifu na
kufanya kwa utofauti, kuwa mvumilivu na king’ang’anizi, kutokukata tamaa
na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa. Siri hizi huwa zinahubiriwa na
kila mtu, na zipo wazi, japo siyo kila mtu anayeweza kuzifanyia kazi.
Kuna
siri moja ya mafanikio ambayo ni muhimu sana, lakini hakuna anayechukua
muda wake kukusisitizia kama ilivyo kwa siri nyingine za mafanikio.
Ukiielewa siri hii moja na kuifanyia kazi, utaweza kuwa mbali sana na
wengine inapokuja kwenye swala la mafanikio.
Kabla
sijakuambia siri hiyo muhimu na hatua za kuchukua ili kuifaidi siri
hiyo, hebu kwanza nikuoe mfano wa hatua ambazo umekuwa unachukua.
Hebu niambie, ni wakati gani ambapo huwa unaweka malengo na mipango yako ya mwaka?
Najua
jibu lipo wazi, wakati wa mwaka mpya, ndiyo huwa unafanya hivyo. Wakati
huo kila mtu anakuwa anazungumzia malengo na mipango mikubwa, hivyo na
wewe unabebwa na mkumbo huo, na kujikuta unaweka malengo na mipango
ambayo siyo yako. Malengo na mipango unayojiwekea wakati wa mwaka mpya
inakuwa siyo yako kwa sababu unaingiliwa na ushawishi wa wengine ambao
nao wanafanya hivyo.
Ndiyo
maana mwezi mmoja baada ya mwaka kuanza, asilimia 90 ya watu wanaokuwa
wamejiwekea malengo na mipango ya mwaka huo, wanakuwa wameshaachana nayo
na kurudi kwenye maisha ya kawaida.
Sasa
siri kubwa ya mafanikio ninayokwenda kukushirikisha hapa leo, inakwenda
kuondoa kabisa hali hiyo ya kuweka malengo na mipango kwa kufuata
mkumbo, na kuweza kufanya jambo hilo muhimu ukiwa na utulivu wa ndani.
Rafiki
yangu mpendwa, sasa umefika wakati wa mimi kukupa siri pekee ya
mafanikio ambayo hakuna anayekusisitizia sana. Siri hiyo ni hii; kwa
chochote unachofanya, kuwa mbele ya wengine.
Hiyo
ndiyo siri, kuhakikisha kila unachofanya basi uko mbele ya wengine.
Kwenye kazi, biashara, maisha, kila kitu, kuwa mbele kabisa ya wengine.
Usikubali kufuata mkumbo au kuwa katikati ya kundi kubwa la watu, wewe
kuwa mbele kabisa, na waache wengine wote nyuma.
Unapokuwa
mbele ya wengine, unaona vizuri kule unakokwenda kuliko ukiwa katikati
ya kundi kubwa la watu. Pia juhudi unazoweka haziingiliwi na usumbufu wa
wengine. Mipango unayoweka inakuwa yako kweli na juhudi unazochukua
zinaendana na mipango hiyo.
Jinsi ya kuitumia siri hii kufanikiwa zaidi.
Rafiki,
kila mwaka nimekuwa nakushauri kuweka malengo na mipango yako mapema
kabla ya wengine hawajaanza kufanya hivyo. Hii ndiyo siri ya kuwa mbele
ya wengine.
Kwa
kuwa kila mtu huwa anaweka malengo na mipango yake ya mwaka mzima mwezi
januari, ambapo kila mtu anakuwa anafanya hivyo, mimi nimekuwa
nakushauri wewe kuwahi kufanya zoezi hilo. Na muda sahihi kwako kufanya
zoezi hilo ni mwezi novemba.
Yaani
malengo na mipango yako ya mwaka 2020 hupasi kuiweka januari 2020,
badala yake unapaswa kuyaweka mwezi novemba 2019. Hii inakusaidia kuwa
na utulivu wakati wa kuweka malengo yako na kutokusumbuliwa na msukumo
wa nje. Lakini pia inakupa muda mzuri wa kukutosha wewe kuanza kufanyia
kazi malengo yako kabla ya wengine.
Na
kizuri zaidi kwenye mfumo huu ni kwamba, mwisho wa mwaka watu wengi
huwa wanapunguza sana juhudi wanazoweka, na hivyo kama wewe ndiyo
umeweka malengo yako, na kuanza kuyafanyia kazi mwisho wa mwaka, unakuwa
na uwanja mpana wa kufanya vizuri kwa sababu wengine wote wanakuwa
wamechoka na kupunguza kasi.
KARIBU TUUANZE PAMOJA MWAKA MPYA 2020.
Kupitia
dhana hii ya kuuanza mwaka mpya mapema, tumekuwa na semina za mwaka
kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Inapofanyika semina hii ndiyo wakati sahihi
kwetu kuuanza mwaka mpya wa mafanikio.
Na
katika kuuanza mwaka mpya wa 2020 kwa mafanikio zaidi, tarehe
03/11/2019 tutakuwa na semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambapo
tunakwenda kuuanza pamoja mwaka wa mafanikio 2019/2020.
Wakati
wengine wameshapumzika na kujiambia wataanza vizuri mwaka 2020
utakapoanza, sisi tunakwenda kuuanza mwaka huo kwa moto mkubwa, miezi
miwili kabla wengine hawajastuka kutoka kwenye usingizi waliolala.
Karibu
sana kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambapo pamoja na kupata
nafasi ya kuuanza mwaka wa mafanikio mapema, utakwenda kujifunza na
kuhamasika kupitia masomo mbalimbali yatakayokuwepo kwenye semina hii
pamoja na shuhuda za wengine ambao wanachukua hatua mbalimbali.
Kama nilivyokushirikisha hapo juu, semina itafanyika siku ya jumapili, tarehe 03/11/2019, jijini Dar es salaam.
Ada ya kushiriki semina hii ni tsh laki moja (100,000/=) na unapaswa kuilipa kabla ya tarehe 31/10/2019.
Ili
kuhakikisha hukosi semina hii muhimu sana kwako kwenda kuanza mwaka wa
mafanikio wakati wengine bado wamelala, unapaswa kutuma ujumbe wenye
majina yao na kwamba utashiriki semina hii. Ujumbe utume kwenda namba
0717396253.
Karibu
sana rafiki yangu tuuanze mwaka mpya 2020 mapema wakati wengine bado
hawajafikiria kufanya hivyo, na hilo linatuwezesha sisi kuwa mbele ya
wengine na hivyo kutokusumbuliwa na fujo zao. Tuma sasa ujumbe wa
kujiwekea nafasi ya kushiriki semina hii, ujumbe uende kwenye namba
0717396253.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala
Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu,
Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha
Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
|
Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.
Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.
Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.
Kama
bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno
KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)
Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha
Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.