Akito taarifa kwa vyombo vya habari afisini mwake punde tu
baada ya kuzuru shule hiyo na kuagiza kufungwa kwake,mkuu mpya wa elimu kwenye
kaunti ndogo ya Koibatek Simon Peter Kemei anasema wanafunzi wapatao 103 wa
shule hiyo sasa watajiunga na shule ya msingi ya St Patrick Shimoni bila
masharti yoyote,huku watahiniwa wa KCPE kwenye shule hiyo wakitrajiwa kukalia
mtihani wao katika shule ya msingi ya Githioro.
Kemei anasema shule hiyo ilijengwa pasipo kuzingatia usalama
wa watoto,huku sita kati ya walimu wa shule hiyo wakihudumu licha yao
kutosjiliw na tume ya wlimu nchini TSC.
Chini ya ufadhili kutoka kwenye wakfu wa Bill Gates na pia
mhasisi wa mtandao maarufu wa FACEBOOK Mark Zuckerberg,shule za Bridge
International zilianzishwa nchini Kenya mwaka wa 2007 kwa lengo la kuhakikisha
kwamba kupitia kwa muungano wao na shule za serikali,watoto wote wanaweza
kupata elimu ya kisasa,na kwa gharama ya
chini kote mashinani.
Shule hizo zenye makao yake makuu jijini Nairobi pia
zinahudumu nchini Uganda ,Nigeria, India,na Liberia.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.